KCSE Past Papers 2021 Kiswahili Karatasi ya 3

KCSE Past Papers 2021 Kiswahili Karatasi ya 3 (102/3) 


Kenya Certificate of Secondary Education Kiswahili Karatasi ya 3

SEHEMU A : TAMTHILIA


P.Kea:Kigogo

1. Lazima

(a) “Aikose? Asiya ni mwanamke halisi bwana! Amemweka Bi Husda hapa.” (i) Eleza muktadha wa dondoo hili. (alama 10)

(ii) Eleza vipengele viwili vya kimtindo alivyotumia msemaji kufanikisha uwasilishaji wa ujumbe.(alama 2)

(iii) Fafanua sifa nne za anayeambiwa maneno haya.(alama 4)

(b) “Kuzorota kwa maadili kunachangia kuzorota kwa mahusiano ya kijamii.” Thibitisha kauli hii kwa kurejelea tamthilia ya Kigogo. (alama 10)

SEHEMU B: RIWAYA

A. Matei: Chozi la Heri Jibu swali la 2 au la 3.

2. Jadili nafasi ya mwanamke katika kuendeleza ukiukaji wa haki za kibinadamu katika riwaya ya Chozi la Heri. {alama 20)

3. (a) Changanua mtindo katika dondoo lifuatalo:

“Una babati sana mweozangu,” alisema Kairi siku moja, ‘Wewe hujapitia tuliyopitia. Tulitendwa ya kutendwa. Siku hiyo tulipofurushwa kwetu kama takataka tulitanga na njia bila kujua tuendako mama mbele, sisi nyuma, mama amebeba kitindamimba ambaye baadaye alishindwa kukamilisha safari; roho yake changa ikakatika papo hapo mgongooi mwa mama, amemezwa na njaa na ugonjwa wa udhaifu wa mapafu. Mama alituelekeza kando ya njia, tukaingia kichakani kiasi. Sijui alikotoa kiserema alichokitumia kuchimba kaburi lenye kina cha haja, tukaufukia mwili wa ndugu yetu huku kilio cha uchungu na jitimai kikihanikiza kote”.

(b) Jadili nafasi ya wahusika wafuatao katika kuijenga riwaya ya Chozi la Herr:

(i) Cizarina

(ii) Tila

SEREMU C: HADITHI FUPI


A. Chokocho na D. Kayanda (Wah.): Tumbo Lisiloshiba na Hadithi Nyingine

Jibu swali la 4 au la 5.

4. A. Chokocho: Masharti ya Kisasa

“Alipokuwa kguu na njia akimwinda kama kunguru ... Ajabu lakini, kwa nini misumari ya nyuki inamwuma sasa ila si wakati ule wa tamaa ya ushindi ilipokuwa mbali ...”

(a) Eleza muktadha wa dondoo hili.(alama 4)

(b) Bainisha toni katika kauli hii. (alama 2)

(c) Fafanua “misumari ya nyuki” kwa kurejelea hadithi: Masharti ya kisasa. (alama 14)

5. (a) “Suala la uozo wa kijamii limejitokeza katika hadithi: Mame Bakari.” Thibitisha.(alama 10)

(b) Jadili mchango wa wazazi katika maisha ya vijana kwa kurejelea hadithi: Ndoto ya Mashaka. (alama 10)

SEHEMU D: USHAIRI


Jibu swali la 6 au la 7.

6. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maSwali.

Mtu asiye heshima, aibu ya roho yake Mfano wake tazama, kama popo mwendo wake Wanaposhindwa wanyama, hudai ndege wenzake Na ndege sio wenzake, wanaposhinda wanyama.

Na siku ya mapatano, ya ndege na wanyama Yeye huwa ni miguno, halipati la kusema Hana masikilizano, kwa ndege wala wanyama Mtu kamaye daima, ni aibu kubwa mno.

Huwa hatamki neno, kama kinywa kimetuna Hapati la mnong'ono, heshima hanayo tena Hana heshima ya neno, wala heshima ya jina Hapati kuonekana, hampi mtu mkono.

Hafai kuandamana, mtu huyo umwepuke Kama alivyo hiana, juu ya nafsi yake Na salama kwako hana, afadhali mtanuke Hiana na roho yake, kwako hawi muungwana.

Mbaya mtu hiana, kuwa naye utajuta Dunia ikikubana, na kusongwa na matata Atakutupa mchana, mbinguni hakuna nyota; Ni mambo yanatukuta, na kisha hutendekana.

(S. Robert)

(a) Eleza ujumbe wa shairi hili.(alama 4)

(b) Bainisha nafsineni ya shairi hili.(alama 2)

(c) Fafanua umuhimu wa uhuru wa kishairi uliotumiwa katika shairi hili.(alama 6)

(d) Eleza dhima ya aina mbili za urudiaji zinazojitokeza katika shairi hili.(alama 4)

(e) BainÄ°sha tamathali za usemi katika ubeti wa kwanza na wa pili.(alama 2)

(f) Andika ubeti wa mwisho kwa lugha ya nathari.(alama 2)

7. Soma shairi lifuatalo kisha ujibu maswoli. Nalilia mazingira yetu haya Hakuna kilicho safi Vyote ni kombo Mrama vimekwenda.

Tazama mto huu Mto utambao katikati mwa jiji kuu Jiji la uzungu na usasa Lenye warembo na wakwasi Wanaolivuka bila fahamu Wmaolilima bila kujali Wanalifumbia macho ilhali lipo!

Najua mwakani watakuja usafi kulitia Usafi ndugu wa siku moja Eti kuupa mji sura! Wanaukosha mji, si mto!

Ni mto ulioona mengi na makubwa kushuhudia Lakini kwa kimya ndugu zangu unakwenda Labda kwa uchovu na bughudha Ningekuwa mimi ningepaaza sauti: “Punguzeni bughudha. Msinitwike mizigo yenu

Maana mimi mnanibebesha mizigo yenu Na minyororo ya uchafu kunitia Kusudi mpate safika. Tangu lini Mto kukoshwa kwa sabuni? Hamjui Mto husafisha dhambi?”

Lakini nionavyo ndugu Taswira ya mto huu Ni taswirn kamilifu ya kizazi chetu! Kizazi baina ya kilichopita na kijacho. (Limenukuliwa kutoka: Tunu ya Ushairi)

(a) Eleza ujumbe wa shairi hüi.(alama 5)

(b) Onyesha mbinu mbili za uhuru wa kishairi katika shairi hili.(alama 2)

(c) Bainisha vipengele vifuatavyo vya kimtindo katika shairi hili.(alama 3)

(i) Tashihisi

(ii) Swali la balagha

(d) Onyesha aina mbili za unıdiaji zinazojitokeza katika ubeti wa pili.(alama 2)

(e) Bainisha nafsineni kstika shairi hili.(alama 1)

(f) Fafanua aina tntu za taswira kwa kurejelea shairi hili.(alama 3)

(g) Eleza toni ya shairi hili.(alama 3)

(h) Andika ubeti wa tatu katika lugha ya nathari.(alama 2)

SEHEMU E: FASIHI SIMULIZI


8. Soma hadithi ifuatayo kisha ujibu maswali.

Hapo zamani za kale Nungunungu na Fisi walikuwa marafıki wa kufa kuzikana. Walizilea familia zao pamoja. Nungunungu aliwafaa watoto wa Fisi kwa nafaka naye Fisi aliwafaa wa Nungunungu kwa nyama. Wanyama wengi waliuhusudu urafiki wao. Hata hivyo, Sungura hakusita kumtahadharisha Nungunungu mara kwa mara.

‘Wdugu,” Sungura alisema, siku moja, “Sijui kilichokuvuta kwa huyu mwenzako, ila nataka ujue kwamba mla mizoga haaminiki, haitakuwa ibra watoto wako wakigeuzwa kitoweo chake.”

Nungunungu aliyatia maneno ya Sungura kwenye mizani, akataka kuyaamini, lakini moyo wake ukamuasa dhidi ya haya. Unajua tena mjukuu wangu kauli za mwenye hila haziSftdÄ°kÃŽkÄ° kWa urahisi. Nungunungu alijisemea moyoni, “Simtarajii ndugu yangu huyu aniendee kinyume.

Nimeishi naye kwa miaka mingi, nikimfaa kwa jua naye akinifaa kwa mvua, tukizungumza ya kupwa na kujaa, tukilizana kwa furaha na simanzi. Itatokeaje anisaliti baada ya muda wote huu? Na iwe hiyo tamaa wamsingiziayo lakini kuwafanya kitoweo watoto wangu mimi ambaye hujisabilia kuwalea watoto wake mwenyewe anapomezwa na msitu akitafuta mizoga! Haiwezekani. La! Hasha!”

Basi mjukuu wangu Nungunungu aliyatia masikio nta; akapuuzilia mbali ushauri wa jirani yake Suun Hakuona haja ya kuufuata ushauri huu kwani alijua kwamba ikiwa kweli Fisi alikuwa na doa, ukweli ungemdondokea viganjani mwake.

Mbivu na mbichi ilibainika wakati kiangazi kikubwa kilikumba kijiji walikoishi Nungunungu na Fisi. Ukame ulibisha hodi. Njaa na ukosefu wa maji ukatishia kukipukutisha kizazi kizima eha wanyama.

Hata hivyo, Nungunungu hakuwa na wasiwasi. Unaweza kusema kwamba yeye alikuwa kondoo mwenye manyoya tele. Maghala yake yalishiba yakatapika nafaka. Hivyo mng'ato wa ukame haukumwathiri.

Kiangazi kilizidi kung'ata naye Nungunungu akaanza kuona muujiza wa kupungua kwa nafaka ghalanisiku baada ya siku. Alipomuuliza Fisi, Fisi alikuja juu. ‘fani mwingine ila yule goigoi, Sungura? Mimi kila mara hujituma kuitafuta mizoga, japo mizoga yenyewe imeadimika.Jakati mwingine hulazimika kujiulia mwenyewe.”

sungura aliposikia hayo alijinyamazia tu. Alijua kwamba za mwizi ni arobaini. AlimwambiaNungunungu, “umdhaniaye ndiye siye.” Kisha akaondoka. Jioni hiyo Sungura alitia gundi kwenyelango la ghala la Nungunungu na kujiendea zake kulala. Alfajiri mbichi Nungunungu aliamshwa na sauti ya kite. Alipotoka nje alimpata Fisi Jo iing'inia ghalanihivi, likawa life la “Mwenye macho haambiwi tazama.” Mjukuu wangu, ingekuwa wewe ungemfanyia nini rafiki yako huyu wa dhati?

Hadithi yanguinaishia hapo. Naomba mbuzi wangu wale majani mabichi na wako wafe wa kiangazi.

(a) (i) Ainisha Rgeno hii kwa kurejelea kigezo cha wahusika. (alama 2)

(ii) Fafanua mbinu site ambazo mtambaji ametumia kuufanikisha uwasilishaji wa ngano hii. (aıama 6)

(iii) Eleze shughuli tatu za kiuchumi ambazo zimejitokeza katika utungo huu. (alama 3)

(iv) Eleza majukumu manne ya fomyula ya kumalizia katika utungo huu. (alama 4)

(b) Kipera cha ngano kinaendelea kufifa katika jamii yako. Pendekeza mbinu tano ambazo jamii yako inaweza kutumia kukinga dhidi ya hali hii. (alama 5)

Post a Comment

0 Comments